AY KWENYE REMIX YA “THE ONE & ONLY” YA NAVIO
Baada ya msanii wa Uganda kwa jina la Daniel Kigozi alias Navio kutamba na single iitwayo “The One & Only” katika vituo mbalimbali vya Radio na Television ndani ya Uganda na Africa Mashariki kwa ujumla sasa imefika tyme ya kutoa remix hiyo.
Kwani hapo awali kuliwa na Mpango wa msanii AY kurekodi collabo yenye ujazo na msanii Navio kutoka nchini Uganda umekaa sawasawa ambapo kazi hii itafanyika bila wasanii hawa kukutana kwa mujibu wa maelezo ambayo AY aliyatoa hapo awali.
Navio ambaye ni rapper anayeiwakilisha vizuri sana Uganda katika anga za kimataifa, ndiye aliyetoa wazo la collabo hiyo na amefanya hivyo kwa kumtumia AY sauti yake amalize kazi akiwa hapa hapa Bongo, ikiwa ni mwendelezo wa mpango wa Navio kufanya kazi na wasanii wote wakali kutoka nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Sasa siku ya leo kupitia his Official Facebook page, Navio amethibitisha kuwa collabo hiyo tayari imekamilika na leo ndio itaanza kusikika kwenye masikio ya watu wakiwa na wasanii wengine kama Papito na Inoss toka Congo.Hivyo mashabiki wa Ay na Navio mkae tayari kusikia remix hii ya “The One & Only” kwani ni collabo inayowakutanisha wasanii ambao wanajua kile wanachokifanya kutokana na uzoefu mkubwa na ukongwe wao katika muziki.
Hii ndio post ya Navio kuthibitisha kutoka kwa remix hiyo:
Post a Comment